1 Timothy 4:1-6

Maagizo Kwa Timotheo

1 aRoho asema waziwazi kwamba katika siku za mwisho baadhi ya watu wataiacha imani na kufuata roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani. 2 bMafundisho kama hayo huja kupitia kwa waongo ambao ni wanafiki, hali dhamiri zao zikiungua kwa kuchomwa moto. 3 cWao huwakataza watu wasioe na kuwaagiza wajiepushe na vyakula fulani, ambavyo Mungu aliviumba ili vipokewe kwa shukrani na wale wanaoamini na kuijua kweli. 4 dKwa maana kila kitu alichokiumba Mungu ni chema, wala hakuna kitu chochote cha kukataliwa kama kikipokewa kwa shukrani, 5 ekwa sababu kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.

Mtumishi Mwema Wa Isa Al-Masihi

6 fKama ukiwakumbusha ndugu mambo haya, utakuwa mtumishi mwema wa Al-Masihi Isa, uliyelelewa katika kweli ya imani na yale mafundisho mazuri uliyoyafuata.
Copyright information for SwhKC